Khalidi Magari Dodoma Mjini tunakupa huduma ya ukaguzi na tathmini ya gari ili kukusaidia kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya gari kabla ya kulinunua.
NI VITU GANI VINAVYOANGALIWA?
Katika ukaguzi wa gari, maeneo yanayoweza kufanyiwa uchunguzi ni pamoja na:
- Hali ya injini
- Mfumo wa gia
- Mfumo wa breki
- Mfumo wa umeme
- Hali ya body na rangi ya gari
- Mfumo wa suspension
- Matairi na mifumo mingine muhimu ya gari.
KWA NINI UKAGUZI WA GARI NI MUHIMU?
- Kufahamu hali ya gari: Unapata taarifa muhimu kuhusu hali ya gari kabla ya kununua.
- Kubaini changamoto zilizopo:Unapata nafasi ya kufahamu kasoro au maeneo yanayohitaji uangalizi.
- Kufanya maamuzi yenye taarifa: Unapata msingi mzuri wa kuamua kama gari linafaa kuendelea na mchakato wa ununuzi.
- Kuelewa mahitaji ya matengenezo: Unapata uelewa kuhusu maeneo yanayoweza kuhitaji matengenezo au uangalizi.
Usifanye maamuzi kwa kuangalia muonekano pekee.Wasiliana nasi ili tuweze kulifanyia gari lako ukaguzi.